Jumanne 13 Mei 2025 - 13:27
Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli akutana na Ayatollah al-Udhma Sistani huko Najaf Ashraf

Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli alifanikiwa kufika katika makazi ya Ayatollah al-Udhma Sistani katika mji mtukufu wa Najaf, na kukutana na yeye kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye.

Shirika la Habari la Hawza - Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli, asubuhi ya siku ya Jumatatu, alifika katika makazi ya Ayatollah al-Udhma Sistani katika mji mtukufu wa Najaf, na kukutana naye kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya pamoja.

Katika kikao hicho, Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli alimkabidhi Ayatollah al-Udhma Sistani nakala kamili ya tafsiri adhimu ya "Tasnīm" yenye juzuu 80, na kama mfano alimkabidhi mwenyewe juzuu ya themanini kwa heshima, naye Ayatollah Sistani aliipokea kwa heshima kubwa na uangalifu maalumu.

Ayatollah al-Udhma Sistani, sambamba na kumkaribisha na kuonyesha furaha kwa kufanikisha kwake kufika katika maeneo matukufu ya Kiislamu, aliitaja tafsiri ya "Tasnīm" kuwa ni fahari kwa Mashia na akasema: "Ninyi mmekuwa katika hifadhi ya Qur'an Tukufu kwa kipindi cha miaka 40 na mmefanya juhudi kubwa; na kazi hii yenu ni fahari kwa Mashia."

Akaongeza kusema: “Asili na mhimili ni Qur'an Tukufu; riwaya za Ahlulbayt (as) ni lazima zilinganishwe na Qur’an, na ni pale tu zitakapokuwa zinapatana na Qur’an ambapo zitakuwa na mashiko na zinaweza kutegemewa na kufanyiwa kazi.”

Alisisitiza: “Mtazamo wetu kwa Hawza ya Qom hauna tofauti na mtazamo wetu kwa Hawza ya Najaf, na kwa kadiri ya uwezo wetu, tutafanya kila tuliwezalo kwa ajili ya Hawza.”

Vilevile, kwa kuonyesha furaha yake kutokana na kikao hicho, alimwambia Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli: “Sifa zenu na athari zenu za kielimu tumekuwa tukizisikia sana, lakini kusikia, kwa hakika si sawa na kuona!”

Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli pia, kwa kumtukuza Ayatollah al-Udhma Sistani kwa cheo chake cha kipekee, alisema: “Uwepo wa shakhsia mkubwa kama wewe ni neema kubwa kwa Hawza na kwa jamii ya Kiislamu. Wewe kwa Mashia na watu wa Iraq ni kama baba mwenye huruma na upole. In shā’ Allāh kivuli chako kitaendelea kudumu.”

Akaongeza kwa kuashiria nafasi ya kipekee ya Marjaiyyah katika nchi ya Iraq: “Hawza ya Najaf, iwe kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, imekuwa chanzo cha baraka nyingi katika ulimwengu wa Kiislamu, na nafasi yako katika kuhifadhi mfumo wa kijamii na kukabiliana na mitazamo ya itikadi kali kama ya Daesh (ISIS) ni nafasi ya kihistoria na ya kudumu.”

Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli pia alitoa shukrani na pongezi kwa huduma kubwa zinazotolewa na Ayatollah al-Udhma Sistani kwenye Hawza, ndani na nje ya Iraq, na akasisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano zaidi baina ya Hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha